Mkanda wa jeshi (shingles) ni jina linalotumika mtaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa vyenye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili. Ingawa vijipele vya mkanda wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili, mara nyingi hupenda kuota kifuani, shingoni, usoni, mgongoni na mikononi.
Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea. Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto. Aghalab ugonjwa huu humrudia mtu zaidi ya mara moja.
Mkanda wa jeshi huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa, zaidi ya miaka 50, utafiti ukionyesha kuwa zaidi ya nusu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 hupatwa na mkanda wa jeshi. Vilevile huwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopunguza kinga za mwili, kama vile, UKIMWI na saratani. Tiba za mionzi na chemotherapy huweza kupunguza kinga za mwili za mgonjwa na kumfanya awe kwenye hatari kubwa ya kupata mkanda wa jeshi.
Mkanda Wa Jeshi Husababishwa Na Nini?
Mkanda wa jeshi husababishwa na kirusi aitwaye varicella-zoster, kirusi yule yule anayesababisha tetekuwanga(chickenpox). Varicella-zoster ni moja ya kundi la virusi waitwao herpes viruses, likijumisha virusi wanaosababisha mafua na vipele vya sehemu za siri. Mtu yeyote yule ambaye alishawahi kupatatetekuwanga anaweza kupata mkanda wa jeshi. Baada ya kupata tiba ya tetekuwanga na kupona, virusi hawa wanaweza kuingia kwenye mishipa ya mfumo wa fahamu na kutulia kimya kwa miaka kadhaa. Baadaye virusi hawa huamka na kusafiri kupitia mishipa ya fahamu hadi kwenye ngozi – na kusababisha mkanda wa jeshi. Hii ndiyo sababu ya ugonjwa huu kuitwa kwa jina jingine la herpes-zoster. Sababu za kurudiwa na ugonjwa huu baadaye hazijawa bayana lakini huenda hii inatokana na kuwa kinga dhidi ya maambukizi hupungua umri unapokuwa mkubwa.
Mtu mwenye mkanda wa jeshi anaweza kumwambukiza mtu mwingine ambaye mwili wake hauna kinga dhidi ya tetekuwanga au kinga ya mwili isipokuwa imara.
Hii itatokea pale mtu huyo atakapogusa vipele vilivyo wazi vya mkanda wa jeshi, mtu huyu aliyeambukizwa, badala yake, ataugua tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.
Dalili Za Mkanda Wa Jeshi.
Mkanda wa jeshi mara nyingi huathiri sehemu ndogo ya upande mmoja wa mwili. Vitu ambavyo vinaweza kujitokeza ni pamoja na:
. Maumivu, kuwaka moto, kufa ganzi na vitu kuchezacheza.
. Maumivu sehemu husika ikiguswa
. Malengelenge
. Kuwashwa
Pamoja na dalili hizo mtu atasikia:
. Homa
. Maumivu ya kichwa
. Hali ya kutopenda mwanga
. Uchovu
Maumivu yatetegemea sehemu ambayo vipele hivyo vimeota, yanaweza kuwa ya kawaida au makali sana. Maumivu haya yanaweza kuchanganya sana ikadhaniwa kuwa mtu huyu ana matatizo ya moyo, mapafu au figo. Watu wengine hupatwa na maumivu haya hata kabla ya kutokwa na vipele.
Kikawaida, vijipele vya mkanda wa jeshi huota kama tabaka (mkanda) la malengelenge linalozunguka upande mmoja wa mwili kuanzia kifuani. Vipele vya mkanda wa jeshi vyaweza kujenga kuzunguka jicho moja, upande mmoja wa shingo au uso.
Tiba Ya Mkanda Wa Jeshi.
Lakini kuna tumaini kwamba unaweza kuondoka na mkanda wa jeshi baada ya kugundua kwamba seli za mwili zikipata chakula chake na kuanza kuzaliana upya, kinga ya mwili ikawa imara. Mpaka sasa suluhisho pekee lililopo ni matumizi ya virutubisho (food supplements, vitamins and minerals, phytonutrients) ambazo hutumiwa kwa kipindi cha miezi sita. Hii itakusaidia kurudi katika hali yako ya kawaida kama jinsi mwenyezi alivyokuumba.
Kwa wanaohitaji ushauri wa bure zaidi kuhusu mkanda wa jeshi wasiliana nasi kupitia WhatsApp/ Call +255714560991.
0 Comments