FAHAMU KUHUSU MCHOCHOTA WA INI AINA B - HEPATITIS B.

Hepatitis B ni maambukizi mabaya sana ya kirusi aitwaye hepatitis B virus (HBV) kwenye maini. Kwa watu wengine ugonjwa huu huweza kuchukua zaidi ya miezi 6 (chronic). Ugonjwa huu ukichukua muda mrefu unaweza kuleta madhara ya kufeli kwa ini, kansa ya ini au liver cirrhosis hali ambayo itaacha makovu ya kudumu kwenye maini. Watu wengi wanaougua ugonjwa huu hupona kabisa. Ukishaambukizwa yafaa kuchukua tahadhari za kusaidia kutowaambukiza watu wengine.

Dalili Za Hepatitis B.
Dalili za hepatitis B huanza kuonekana baada ya mwezi mmoja hadi minne baada ya kupata maambukizi, nazo ni:

I. Maumivu ya tumbo.
II. Mkojo mweusi.
III. Homa.
IV. Maumivu ya joints.
V. Kukosa hamu ya kula
VI. Kichefuchefu na kutapika
VII. Udhaifu wa mwili na mwili kukosa nguvu
VIII. Macho na ngozi kugeuka rangi na kuwa vya njano

Chanzo Cha Hepatitis B.
Ugomjwa wa hepatitis B husababishwa na kirusi aitwaye Hepatitis B virus (HBV). Kirusi huyu huambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia damu, shahawa na maji maji mengine ya mwilini. 

Njia kuu za uambukizaji zikiwa:
I. Kujamiiana. 
Unaweza kuambukizwa na mtu mwenye ugonjwa huo kama utajamiiana naye bila kutumia kinga na damu, mate, shahawa au maji maji ya ukeni yakaingia ndani ya mwili wako.

II. Kuchangia sindano. 
Kirusi wa hepatitis B anaambukiza kirahisi sana kupitia sindano zenye damu ya mtu mwenye virusi hivi.

III. Mama kumwambukiza mtoto. 
Mama mwenye mimba mwenye virusi vya HBV anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa tendo la uzazi. Mtoto anaweza kupewa chanjo baada ya kuzaliwa na akaepuka kuambukizwa, hivyo ni vizuri kuchukua tahadhari ya kujipima wakati una ujauzito.
Hepatitis B hugawanywa katika makundi mawili; Hepatitis ya muda mfupi (acute hepatitis) na hepatitis ya muda mrefu (chronic hepatitis).
Acute hepatitis B:
Hii huchukua chini ya miezi 6 kupona. Kinga zako za mwili zinaweza kupambana na kuuondoa ugonjwa huu na ukapona kabisa katika muda mfupi. Watu wazima mara nyingi huugua acute hepatitis ingawa mara chache huweza kufikia kuwa chronic hepatitis.

Chronic hepatitis B: 
Ugonjwa huu huchukua miezi 6 au zaidi kupona. Kama kinga za mwili wako hazitaweza kuushinda, basi ugonjwa utakuwa ni wa maisha kwako na uwezekano wa magonjwa makubwa zaidi kama ya cirrhosis na saratani ya ini ukiongezeka. Chronic hepatitis B inaweza isigundulike kwa miaka mingi hadi mgonjwa atakapokuwa mahututi kutokana na ugonjwa huu wa homa ya ini.

Madhara ya hepatitis B
Kuwa na hepatitis B kwa muda mrefu (chronic hepatits) kunaweza kusababisha madhara makubwa yafutayo;

I. Makovu kwenye ini (Cirrhosis). 
Kuvimba kwa ini kwa muda mrefu kunakotokana na virusi wa hepatitis B kunaweza kusababaisha makovu kwenye ini (cirrhosis) na kulifanya ini lishindwe kufanya kazi yake inavyotakiwa.
II. Saratani ya ini. 
Watu wenye hapatitis B kwa muda mrefu wanaweza baadaye wakapata saratani ya ini.

III. Ini kufeli. 
Ini likishindwa kufanya kazi zake kabisa, hatua nyingine ya kuwekewa ini jingine itahitajika.

IV. Matatizo mengine. 
Mgonjwa mwenye hepatitis B anaweza kupata matatizo ya figo, uvimbe kwenye mishipa ya damu na upungufu wa damu.

Tiba Ya Hepatitis B.
Kama vipimo vikionyesha kuwa una hepatitis B unahitaji kutumia virutubisho ambavyo vitasaidia kuweka kinga ya mwili kuwa imara na kufanya seli za mwili kuzalisha seli mpya ambazo zitapambana na changamoto hiyo.

Kwa anayehitaji ushauri wa bure zaidi kuhusu Hepatitis B awasiliane nasi WhatsApp/ Call +255714560991.

"Afya yako ni jukumu lako mwenyewe binafsi. Sio la baba, mama, mke, mume, ndugu au daktari. Chukua hatua afya yako iko mikononi mwako."

Post a Comment

0 Comments